Katika muda wa masaa 24 zilizopita taifa sasa limerekodi visa vipya 426 na vya virusi vya corona hii ni kutokana na sampuli 5,168 na kufikisha jumla ya idadi ya 31,441 ya watu walioambukizwa virusi hivyo tangu kisa cha kwanza
Katibu msimamizi wa wizara ya afya Mercy Mwangangi amesema Hayo yakijiri watu 10 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya jumla ya 516 watu walioaga kwa ajili ya corona.
Pia hii leo watu 257 wamepona virusi vya corona na kufikisha idadi ya 17,869 ya watu waliopona kutokana na watu hao 195 wamepona wakiwa nyumbani bali 63 wameruhusiwa kuenda nyumbani kuto hospitali mbalimbali.
Na katika taarifa za kuvunja moyo ni kuwa watu 10 zaidi wamefariki kutokana na virusi hivyo nchini.
Kutokana na maambukizi ya leo mgonjwa wa umri wa chini ana miezi mitatu na mgonjwa wa umri wa juu ana miaka 88.