Papa Leo aomba radhi kwa mchango wa Kanisa katika utumwa

Papa Leo XIV, ameomba msamaha leo kwa nafasi ya Kanisa Katoliki katika kuhalalisha biashara ya utumwa, akisema kuchelewa kulaani mfumo huo imebaki kuwa jeraha katika kumbukumbu ya Ukristo.

Papa Leo XIV, ameomba msamaha leo kwa nafasi ya Kanisa Katoliki katika kuhalalisha biashara ya utumwa, akisema kuchelewa kulaani mfumo huo imebaki kuwa jeraha katika kumbukumbu ya Ukristo.

Katika waraka muhimu unaoonya kuhusu hatari ya aina mpya za utumwa katika uchumi wa kidijitali, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, amesema kuwa taasisi za Kanisa zilimiliki watumwa hadi katika kipindi cha Zama za Kati.

Waraka wake uitwao Magnifica Humanitas yani ubanadamu uliotukuka, pia umegusia kwa upana changamoto za kisasa, ikiwemo athari za teknolojia na akili mnemba kwa utu wa binadamu. Unamulika kwa kiasi kikubwa namna ya kulinda utu wa binadamu wakati ambapo dunia inazidi kutegemea teknolojia ya Akili mnemba.

Viongozi kadhaa wa Kanisa hilo waliopita, waliwahi kuomba msamaha kwa mchango wa Wakristo katika biashara ya utumwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *