visa vya wizi vyaongezeka Uasin Gishu

Onyo kali imetolewa kwa wananchi ambao watapatikana wakijihusisha na uhalifu wa aina yoyote katika kaunti ya Uasin Gishu kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naibu kamishna wa eneo la Turbo Ibrahim Hassan amesisitiza haja ya wenyeji kuishi kwa amani na kujitenga na maswala ambayo yanaweza yakazua vurugu na kuwafukuza wawekezaji jijini Eldoret kuwa wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Kulingana naye,maandamano ya Jumatano hayakuafikia malengo ya maandamano namna katiba inavyonakili ila ilikua njama ya kuvuruga amani kwenye jiji swala analosema watakaopatikana wakikiuka sheria wataadhibiwa.

Ametaka uwaiano na utangamano miongoni mwa wananchi udhihirike ndipo shughuli za maendeleo ziweze kusonga mbele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *