Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametoa wito wa mdahalo baina ya vijana na serikali ili kutanzua maswala tata yanayoshinikizwa na vijana wa kizazi cha sasa almaarufu Gen Z.
Akirejelea maandamano ya hivi majuzi yaliyosheheni visa vya mauaji, uporaji na rabsha zilizoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini askofu amesikitia visa hivyo akitoa wito Amani nchini, kwa kuwa ilivyo kwa sasa nchini ni dhigirisha kuwa taifa ilanelekea pabaya.
Askofu Kimengich kadhalika amewasuta wanasiasa wanaofadhili ghasia hizo kwa lengo la kujipatia umaarufu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 kukoma kufanya hivyo akisema kuwa uchochezi huo huenda ukazamisha taifa kwenye lindi la machafuko.
Amedokeza kuwa taifa la kenya litazidi kusalia nyuma kimaendeleo ikiwa kila wakati wa maandamano kutashuhudiwa visa vya uharibifu na uporaji wa mali katika miji mbalimbali nchini.
