Askofu Kimengich; Ekaristia ni tunu msingi ya karama

jimbo katoliki la Eldoret limeandaa kumbukumbu ya miaka kumi na tatu baada ya matawa Anna wa ekaristia takatifu ambayo imewiana na sherehe ya mwili na damu ya kristu almaarufu Corpus christi.

askofu wa jimbo la Eldoret Dominic Kimengich akihubiri katika sherehe hiyo iliyoandaliwa katika mji wa Ekaristia Burnt forest, ametoa wito kwa kila mmoja kukumbatia maisha ya sakramenti ambayo anasema kuwa huleta uponyaji mkubwa katika maisha ya binadamu kwa kuwa sakramenti hizo ndizo daraja ya kumkaribisha kristu maishani mwao.

askofu amemkumbuka mtawa Anna Ali kama mtu ambaye alifuata kwa ukaribu maisha ya ekaristia na kwamba kifo chake katika kristu utamjalia uzima wa milele, akitoa wito kwa kila moja kadhalika kuiga mfano wa mtawa huyo kwa kujitwika jukumu la kuabudu ekaristia takatifu kila wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *