Msimu wa mvua unapoendelea katika maeneo mengi nchini, hali hiyo imeonekana kuathiri bei ya bidhaa katika soko la manispaa ya jiji la Eldoret.
Kulingana na wafanyabiashara tuliozungumza nao, bei ya bidhaa kama vile vitunguu na nyanya imeongezeka huku ndizi na dania zikipatikana kwa wingi sokoni.
Matunda aina ya tikiti maji, mananasi, maembe, tufaa miongoni mwa mengine, yanauzwa kulingana na ukubwa au vipimo vya uzani kama wanavyotueleza wafanyabiashara Susan Kariuki na Cornellius Rop.
Kwa upande wa Nafaka, mkebe wa kilo mbili wa mahindi makavu yanauzwa kwa Sh. 140 huku gunia la kilo 90 la bidhaa hiyo likuzwa kwa kati ya Sh. 5,900 na Sh. 6,300. Maharagwe aina ya Nyayo, wairimu na saitoti kipimo cha mkebe wa kilo mbili yanauzwa kwa Sh. 350, huku yale ya green yellow, kipimo sawa na hicho yakiuzwa kwa Sh. 500.