Hali ya huzuni ilitanda katika jimbo nzima la Eldoret baada ya paroko wa parokia ya St Mathias Mulumba Tot padre Alois Bett kuawa kwa mtutu wa risasi.
padre Bett alivamiwa na majangili hao siku ya Alhamisi mwendo wa saa saba mchana alipokuwa akiandamana na washiriki waliokuwa wakipokea chakula cha kiroho Jumuiyani katika parokia hiyo, ambapo majangili hao walimmiminia risasi na kufariki papo hapo.
kulingana na askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Lelei ni kuwa ni kisa ambacho kilizua mshangao mkubwa katika jimbo akimtaa padre Bett kama mtu aliyejisadaka bila kujibakisha katika huduma yake ya kichungaji na kwamba kifo chake kimejiri akiwa katika shughuli za uinjilishaji.
hata hivyo idara ya usalama katika eneo la Tot na kaunti ya Elgeiyo Marakwet kwa ujumla ilidinda kuhusisha visa vya mauaji ya padre huyo na wizi wa mifugo ikisema kuwa kwa sasa watu sita wamekamatwa ili kusaidia polisi na uchunguzi kuhusiana na sababu ya mauaji ya padre huyo.
