Wito umetolewa kwa wanafamilia kujiepusha na upangaji uzazi ikiwa kiini cha kudidimia kwa miito mbalimbali katika jamii.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Morris Muhatia Makumba,alisikitia kile anasema kuwa wazazi wengi wamejiingiza katika upangaji wa uzazi kwa kisingizio cha hali ngumu ya uchumi ambayo anasema imechangia kudidimia wa miito mbalimbali kanisani.
Wakati huo,amewashauri wazazi kupalililia miito mbalimbali iwe ya ukasisi,utawa ,kuingia kwenye ndoa ili kuongeza na kuendeleza kizazi kijacho.