Askofu mstaafu wa jimbo katoliki la Kitale Maurice Anthony Crowley ametoa wito kwa wakenya kujiepusha na visa vya mauaji na badala yake kukumbatia mwito wa mazungumzo na kutatua tofauti zao bila kupoteza maisha ya wengine.
Akihubiri katika parokia ya Kuserwo kwenye hafla ya mazishi ya Mzee Smith Churitich askofu amesema kuwa inasikitisha Zaidi kwa taifa la Kenya kushuhudia maovu kama Vila mauaji ya jinsia ya kike nchini.
Ametoa kwa Kila mmoja siku zote kutafakari neno la Mungu siku zote duniani akisema kuwa kifo kwa mzazi mmoja ni pigo kwa mapadre wote.