KCCB:Komesheni mauaji

Baraza la maaskofu katoliki nchini KCCB imetaka uwajibikaji kutoka kwa serikali ya kitaifa kufuatia visa vya mauaji na kupanda kwa gharama ya juu ya maisha nchini.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni askofu mkuu a jimbo kuu katoliki la Kisumu Morris Muhatia Makumba,viongozi hao wa kidini wamesikitikia kile kila kukicha kunashuhudiwa mauaji hasa ya wanawake na hakuna hatua yoyote serikali imechukua kuhakikisha maisha ya mwananchi inalinda ila visa hivyo vinazidi kupanda kila kuchao.

Maaskofu hao vilevile,wanataka serikali kuweka wazi mikakati zilizowekwa kukabili changamoto ambazo zinakumba bima mpya ya afya ya SHA ambayo wanasema,wakenya wameteseka ya kutosha kwani wanaeleza kwamba,wengi wao wamepoteza maisha kwa kukosa matibabu kwa kuwa,SHA haijakubalika vyema kwenye hospitali nyingi nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *