Monsinyori Wallace Ng’ang’a Gachihi sasa atasimikwa kama askofu wa tatu wa jimbo la jeshi tarehe kumi na mbili mwezi wa kumi mwaka huu.
Hii inajiri kufuatia kuteuliwa kwake na Baba mtakatifu Francisko juma lililopita, kuliongoza jimbo hilo la jeshi ambalo limesalia chini ya usimamizi padre John Njue Njeri, na padre mstaafu Benjamin Maswili, ambao wamekuwa wakisimamia jimbo hilo baada ya kustaafu kwa askofu Alfred Rotich, ambaye kwa sasa ni mchungaji wa jimbo katoliki la Kericho.
Haya yanajiri miezi sita tu baada ya Monsinyori Wallace Nganga kuteuliwa na Baba mtakatifu kuwa askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi, uteuzi ambayo ilifanywa tarehe kumi na tatu mwezi wa Februari mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa askofu wa kwanza wa jimbo hilo la jeshi alikuwa mwadhama Maurice Kadinali Otunga, akifuatwa na askofu Alfred Rotich, huku askofu Wallace Nganga akiwa askofu wa tatu kuliongoza jimbo hilo.