Bei mfukoni

Wakulima katika kaunti ya Uasin Gishu walishabikia hatua ya serikali ya kuwahakikisha kwamba  bei ya maziwa inaimarishwa kuanzia mwezi ujao.

Wakizungumza mjini Eldoret  walisema kuwa wamekuwa katika njia panda baada ya serikali hapo awali kuyanunua maziwa yao kwa bei ya chini mno swala ambalo wanasema ilichangia wengi wao kuiasi ukulima wa maziwa.

Wakulima hao sasa waLIsema iwapo juhudi hizo zitaafikiwa watakua na fursa nzuri ya kuwafuga mifugo wengi wa maziwa na kuimarisha maisha yao kupitia kilimo hicho.

Haya yanajiri baada ya naibu wa rais Rigathi Gachagua kuwahakikishia wakulima  kuwa bei ya maziwa itapanda  hadi shillingi 60  kwa lita kutoka shillingi 45  kuanzia  Machi  1,2024 na pia kuhakikishia  wakenya kuwa serikali itaingilia kati na kutenga shillingi millioni 900 kwa kampuni ya KCC kuyanunua maziwa ili kudhibiti bei ya maziwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *