Solai – Nakuru; Hatimaye Kenei Apumzishwa

Afisa wa polisi aliyekuwa mlinzi katika afisi ya naibu wa rais William Ruto, Kipyegon Kenei anatarajiwa kupumzishwa mchana wa leo kwao katika kijiji cha Chemasis kwenye kaunti ya Nakuru.

Naibu wa rais Dkt William Ruto ni kiongozi wa ngazi ya juu kuwasili katika hafla ya mazishi ya sajenti Kipyegon Kenei.

Mwendazke alikuwa ni kiongozi wa ulinzi katika afisi ya Harambee Annex juma moja lililopita akipatikana akiwa amefariki nyumbani kwake.

Kulingana na uchunguzi uliofanyika imepatikana kuwa mwendazake aliuawawa huku kukiwa na jaribio la  kuzuia ukweli kujulikana na jinsi alivyoangamizwa.

Mkurugenzi wa idara DCI George Kinoti amedokeza kuwa wanajizatiti wawezavyo ili kubaini kubaini wale waliotekeleza uovu huo. Wakti huo maafisa wa DCI wanaofanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha afisa huyo, wamewaambia wa waandishi wa habari kuwa waliotekeleza mauaji hayo walishirikiana na afisa mmoja katika kampuni ya Safaricom kuficha ukweli na habari muhimu katika simu yake kufutwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *