Bishop Anyolo; Maslahi ya wakenya yapewe kipaumbele

Viongozi wakuu nchini wametakiwa kuandaa mazungumzo yenye lengo la kusuluhisha matatizo ambyo kwa sasa uyamewasakama wakenya yakiwemo hali ya juu ya kiuchumi miongoni mwa mengine.

Katika hotuba yake kwenye sherehe ya siku ya kifamilia katika dekania ya magharibi jimbo kuu katoliki la Nairobi askofu mkuu wa jimbo hilo Philip Anyolo amesema kuwa huu sio wakati wa malumbano  bali kutafuta suluhu la kudumu akitoa wito kwa rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuweka kando maslahi yao ya kibinafsi na badala yake washiriki mdahalo itakayonifaisha wakenya.

Askofu huyo kadhalika ametoa wito kwa wananchi kutokubali kuchochewa dhidi ya mwingine na mwanasiasa akitaka kila moja kuliombea taifa na kushiriki katika vikao ambavyo yatafanikisha amani humu nchini na hata mataifa ambayo kwa sasa yanakumbwa na misukosuko.

Ametoa wito kwa familia kadhalika kujifunza kusuluhisha matatizo yao kwa njia ya amani pasi na ugomvi akisema kuwa mgogoro ndani ya familia utaathiri jamii kanisa na hata taifa kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *