Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amewataka viongozi wa kisiasa na idara ya usalama hasa katika bonde la kerio kuandaa mkutano na wenyeji ili kujadili mbinu za kupatikana kwa amani.
Akiongea mjini Eldoret askofu Kimengich alisema kwamba kama viongozi wa dini wamejaribu kila wawezalo ila yaonekana kuwa juhudi ambazo viongozi wa dini wameweka kwa miaka mingi hazijaweza kuzaa matunda ila akasema kwamba huenda kupitia mbinu hiyo ya viongozi wa kisiasa maeneo hayo kuandaa mkutano na kupata suluhu la kudumu.
Askofu Kimengich vilevile alieleza kwamba viongozi wa kidini wanastahili kujitokeza na kuendelea kushirikiana na viongozi hao ili kusaidia katika upatikanaji wa amani.
Kadhalika aliwaomba wenyeji kukumbatia mwito wa amani ndipo waweze kupata maendeleo na kuinuka kimaisha.