Ukosefu wa usalama bado unaendelea kushihudiwa katika maeneo yanayopakana na Bonde la Kerio ambapo watu 8 wamepoteza maisha Yao na mifugo kuibwa majuma matatu tu baada ya waziri wa usalama nchini Kithure Kindiki kuzuru bonde hilo na kuwarejesha kazini maafisa wa akiba NPR.
Akitoa kauli yake, gavana wa kaunti ya Elgeyo marakwet Wesely Rotich alisema kwamba njia mwafaka ya kukabiliana na visa hivyo ni kuwapokonya wakazi wanaomiliki silaha haramu katika eneo la bonde la Kerio.
Gavana huyo alisisitiza kuwa Kuna haja ya serkali kutumia mbinu zozote zile kurejesha amani ndipo wenyeji waweze kuendelea na shughuli zao kwa amani.
Kwa upande wake,John Cherwon moja wa wakazi kutoka eneo la Arror, lidokeza kuwa ukosefu wa usalama imechangia pakubwa wao kuhofia maisha yao huku mifugo zaidi 400 zikiibwa.