Wito umetolewa kwa serikali ya kitaifa kuhakikisha imeweka mikakati Ya kutosha kuinua sekta ya elimu na kuona kuwa kila mtoto nchini anapata elimu bila malipo.
Kulingana na askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Momabasa na ambaye pia ni mwenyekiti wa muungano wa maaskofu nchini KCCB Martin Kivuva Musonde ni kwamba kila mtoto wa taifa hili anastahili kupata haki ya kusoma bila malipo ikizingatiwa kwamba wengi wa wazazi hawana uwezo wa kugharamia elimu ya wanao.
Akiongea wakati wa hafla ya kusimikwa kwa askofu wa pili wa jimbo katoliki la Kitale Henry Juma Odonya Askofu Kivuva amesikitikia gharama ambayo elimu kwa sasa inawakuna na kuwanyima usingizi wazazi akisisitiza kuwepo kwa sera za kudumu kuinua elimu nchini.
Alisisitiza kuwa uwepo wa kanisa na kukosoa kwake serikali haimanishi kwamba wanaenda kinyume na yeyeyote bali wanaisaidia katika kufahamu kwamba yapo baadhi ya maswala ambayo huenda wakasahau kutimiza au hata kutilia maanani.
Kadhalika,aliwataka wakenya kutotegemea tu msaada wa chakula kwa waathiriwa wa baa la njaa kutoka kwa seriakli au hata kuagizwa kwa chakula hicho kutoka kwa mataifa za nje bali wawe huru kuwasaidia wenzao bila ya miegemeo yoyote na kuweza kukuza chakula cha kutosha ndipo pesa zinazotumiwa kuagiza chakula hiyo iweze kutekeleza miradi nyinginezo.