RAIS:maendeleo bila mapendeleo

Rais William Ruto amewaonya viongozi waliochaguliwa dhidi ya kushiriki malumbano za kila mara badala ya kuyatekeleza yale waliyochaguliwa kutekeleza kwamba sharti wajitenge nazo.

Akiongea akiwa kwenye ziara katika kaunti ya Bomet Ruto alisema kwamba inasikitisha kushuhudia viongozi ambao wenyeji walitaraji kuwasaidia kupitia maendeleo wakiwa wanangangania vyeo katika kaunti swala analosema sharti likomeshwe mara moja na wao kufahamu lipi linawapasa kufanya.

Rais alisema kisa cha hivi majuzi ambapo viongozi wa kaunti ya Kericho walihusika katika kupigania vyeo katika kaunti hiyo imesababisha kutoendelezwa kwa shughuli zozote katika serikali ya Kaunti akiwataka wawakilishi wadi kujitenga na hayo na kuwasaidia wenyeji kupata maendeleo na kuimarisha uchumi wa kaunti na taifa nzima.

Wakati huo,kiongozi wa taifa aliweka bayana kwamba maswala ya kutopigiwa kura na baadhi ya wananchi nchini sio swala la kuzingatiwa kw akile anasema demokrasia ipo na kila mkenya anauhuru wa kumchagua kiongozi anayemuenzi,hivyo akadokeza kwamba serikali yake itawajumuhisha wakenya wote iwe waliomchagua wale ambao hawakumchagua ilimradi wamefurahia matunda ya uongozi wake ya maendeleo bila mapendeleo yoyote.

Kadhalika,rais amesema kwamba ni fursa ya kila kiongozi nchini kutekeleza jukumu lake wawe walioserikalini au kwenye upinzani maana kila mkenya anahaki kikatiba kutekeleza kile kinachowiana na katiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *