SERIKALI:Chiloba aliuawa

Imebainika kwamba chanzo cha kifo cha mwanamtindo Edwin Kiprotich maarufu Chiloba mwili wake ukiatikana kwenye sanduku ya mabati katika eneo la Kaptinga-Kipkenyo katika kaunti ya Uasin Gishu kwamba alifariki kwa kukosa hewa.

Kulingana na mwanapatolojia mkuu nchini Johannes Odwour aliyeongoza uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa ya Moi Eldoret amesema kwamba haya yamebainika kutokana nawalipata soksi tatu kwenye mdomo wa marehemu na mdomo kufungwa na kitambaa.

Oduor Vilevile alisema kwamba wamechukua sambuli ya mwili huo kuchunguza zaidi kwa kile amesema hawakupata majeraha yoyote kwenye mwili wa mwendazake.

Wakati huo, amekanusha madai kwamba macho ya marehemu yaliyofolewa kwani anasema kwa kawaida maiti ikioza muonekano wa mwili ni tofauti mno.

Kadhalika,mkurugenzi wa hospitali ya Moi Eldoret Dkt.Wilson Arwasa amewaomba wazazi na jamii kwa ujumla kuchukua jukumu la kuwapa mawaidha wanao kwa kile amesema maadili ya watoto imeharibika sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *