Kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Dkt.Eddyson Nyale amesema kwamba idara ya Usalama katika kaunti imeweka mikakati na sera za kutosha kuwakabili wahalifu.
Akiongea mjini Eldoret Nyale alisema kwamba kufuatia msururu wa utovu wa usalama imebainika kuwa baadhi ya vyanzo vya utovu huo ni kupitia kuweka kamera za CCTV kwenye maeneo yote ya umma hasa kuwanasa wahalifu hao.
Kamishna huyo vilevile alisema kwamba watahakikisha wafanyibiashara wanaoendesha biashara ya bodaboda wote wamajiunga na vikundi mbalimbali katika maeneo yao ya biashara ndipo wanaojificha kwa wanabodaboda wakamatwe na kuadhibiwa.
Yamejiri haya baada ya kushuhudiwa utovu wa usalama katika siku za hivi karibuni katika maeneo kadhaa katika kaunti ya Uasin Gishu ambao katika eneo la Naiberi kaunti ndogo ya Ainabkoi kuandamana wakilalamikia utovu wa usalama katika makaazi yao.