ENG.LAGAT:Bishara kuimarika hivi karibuni

Serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu kupitia idara ya Uchukuzi, Barabara na Ujenzi wa Umma imekamilisha kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara katika soko la jumla la mazao ya Kimumu-Bahati ili kuboresha miundombinu sokoni na gavana Jonathan Bii utawala unalenga kuimarisha uhamaji sokoni na kuweka mazingira mazuri ya biashara.

Wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo mnamo Ijumaa, timu kutoka Idara ya Barabara ilithibitisha kuwa kazi ambayo imekamilika kufikia sasa ni pamoja na barabara inayounganisha kutoka sokoni hadi barabara ya Eldoret -Iten iliyoko (Jerusalem) kilomita 0.73 ambapo changarawe nzito imebandikwa.

Kwa mujibu waziri wa barabara za Mhandisi Joseph Lagat, lengo la utekelezaji wa miradi ya barabara kwa wakati ni kuhakikisha miundombinu inaboreshwa ili kurahisisha usafirishaji huru wa bidhaa na huduma katika masoko nchini kote na pia kusaidia wasafirishaji kutoka sehemu za vijijini kupata masoko kwa urahisi, hivyo kuboresha maisha ya wakazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *