MISA YA UASKOFU

Jimbo katoliki la Kakamega liliandaa misa siku ya jumamosi ya kusherehekea miaka hamsini ya daraja la uaskofuĀ  wa askofu mstaafu na mwanzilishi wa jimbo hilo askofu Philip Sulumeti.

Misa hiyo iliongozwa na mwakilishi wa Baba mtakatifu nchini na Sudan Kusini Mwadhama Mathews Herbatus Maria Van Megen, akimtaja askofu Sulumeti kama baba aliyesimamia imani na kujali maslahi ya wwenyeji wa jimbo lake, kwa kujenga shule nyingi na mahospitali mbalimbali katika jimbo hilo.

Akihubiri katika misa hiyo askofu mkuu wa jimbo kuu la Kisumu askofu mkuu Maurice Muhatia Makumba, akimsifia askofu mstaafu Sulumeti kama mtu aliyejisadaka bila kujibakisha katika utendakazi kwenye shamba la Mungu, akimtaja kama mfano wakuigwa katika jamii.

Askofu Sulumeti aliteuliwa kuwa askofu msaidizi wa askofu wa  jimbo la Kisumu De Reeper mwaka wa 1972, na kisha akateuliwa kama askofu wa tatu wa jimbo katoliki la Kisumu, alikohudumu kwa miaka miwili kabla ya kuteuliwa kama askofu mwanzilishi wa jimbo katoliki la Kakamega, mnamo Februari tarehe ishirini na nane mwaka wa 1978.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *