Maafisa wa polisi katika kaunti ndogo ya Kesses katika kaunti ya Uasin Gishu County wameanza shughuli ya kuopoa mwili wa mwanamme mmoja anayeaminika kujiua kwa kujirusha kwenye kisima baada ya kumua mpenzi wake kwa mizozo ya kifamilia.
Inaaminika kwamba mwanamme huyo alimdunga kisu mwanamke huyo mwenye umri wa kati kabla ya kujitoa uhai kw akujirusha kisimani.
Akithibitisha kisa hicho haya kamanda wa polisi katika kaunti ya Uasin Gishu Ayub Gitonga Ali alisema maafisa wa polisi eneo hilo wameanzisha shughuli hiyo huku uchunguzi ukitarajiwa kuanza pindu mwili huo utakapo patikana.
Mwili wa mwendazake umehifadhiwa kwenye makafani ya hospitali ya mafunzo na rufaa Moi Eldoret.