Mzozo wa Ukoo Elgeiyo Marakwet

Zaidi ya wakazi 200 waliopoteza makao kufuatia mzozo wa ardhi katika eneo la Maron eneo bunge la Marakwet mashariki kaunti ya Elgeyo Marakwet wamepata uzaidizi kutoka shirika la msalaba mwekundu.

Wakazi hawa waliweza kupata malazi , hema na vyakula  baada ya zaidi ya nyumba 40 ,  ghala kuteketezwa na zaidi ya ngombe 25 kuibiwa.

Kulingana na mwakilishi wa wadi ya Embobut /Embolo Paul Kipyatich  amekashifu pakubwa kisa hicho akisema kuwa hilo limesababisha hasara kubwa.

Kipyatich vile vile ametaka koo la Kasekei na Kamosombei kusika tofauti zao kwa nyia inayostahili .

Haya yanajiri huku kamishena wa kaunti hiyo Ahmed Omar kutoa onyo kali kwa machifu na manaibu wao kuwatambua wahusika waliotekeleza kitendo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *