Askofu wa dyosisi ya Eldoret Dominic Kimengich amewataka wakenya kuyakubali matokeo ya uchaguzi na kusukuma ghurudumu ya maisha kwa kujishghulisha na kazi ambazo wamebarikiwa nazo.
Alisema kwamba kila shindano lina mshindi na mshindani na yapasa sasa wakenya kwa jumla kuhakikisha kwamba wamefanikisha ndoto zao kwa kurejelea shughuli za kawaida ikzingatiwa hali ya uchumi kwa sasa akieleza kwamba sharti wajikakamua kimaisha kwa mafanikio ya baadae.
Askofu Kimengich aidha,akiwataka wakenya kuzika tofauti zao za kisiasa za hapo awali na kuungana kuinua uchumi wa taifa hili.
Wakati huo,alisema kanisa na viongozi wa dini kila muda wako tayari kuwapokea wakenya ambao wanatafuta mawaidha muda wowote ule watahitaji na milango ya kanisa yako wazi kila mara.