Jimbo katoliki la Eldoret limeandaa mkutano wake wa kwanza kwa baraza la viongozi wa jimbo kutathmini maendeleo ya jimbo na miradi mbalimbali ambayo yanahitaji kukamilishwa wa St.John’S ikiwa mojawapo tangu askofu Dominic Kimengich kupewa fursa ya kuhudumu katika jimbo hili.
Akiongea na kituo hiki kwa njia ya kipekee,Askofu wa jimbo hili la Eldoret Dominic Kimengich alisema kwamba mkutano huo maalum ambao uliongozwa na wanakamati wa parokia zote jimboni walijadili utunzaji wa imani miongoni mwa wakristu kwenye parokia mbali mbali na miradi mbalimbali jimboni.
Kadhalika,Askofu kimengich alisema wasimamizi ambao walikua wanaongoza kupokea maoni ya Synodi jimboni litaanda mkutano wake 6-8 oktoba mwaka huu kujadiliana namna wakristu wamepokea swala hilo na yale ambayo yanahitajika kufanyiwa mageuzi kuwafaa wakristu wote katika jimbo la Eldoret.