Wazazi wamehimizwa kuwakubali wanao wenye changamoto za kimaumbili maana ni Baraka yao kutoka kwa mwenyezi mungu.
Kulinganana na mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Uasin Gishu Harrison Muryuki ni kwamba kila mtoto amebarikiwa kitofauti na yahitaji wazazi kuwaruhusu kutimiza ndoto zao hata kupitia kushiriki michezo mbali mbali shuleni.
Akiongea afisini mwake Muryuki alisema wapo baadhi ya wazazi ambao wamewafungia nyumbani kwa sababu wanahofia kupata aibu kwa hili akisema wanazima ndoto za wanao.
Ameyazungumza haya wakati kaunti ya Uasin Gishu wakiandaa mashindano mbalimbali kwa wanafunzi wenye hitaji katika maisha yao mashindano yatakayo tamatika jumanne juma lijalo.