Kamishna wa kaunti ndogo ya Kapseret James Wambua amewatahadharisha wafanyibiashara wanaoendeleza biashara haramu kwamba siku zao zimehesabiwa.
Akiongea katika mtaa wa Langas Viungani mwa mji wa Eldoret Wambua alisema vijana wengi wamepotoka kimaadili kutokana uraibu wao wa mihadarati na pombe haramu swala analosema litakomeshwa hivi karibuni.
Wambua alisema kwamba wataanza msako mkali katika kaunti ndogo hiyo na mitaa yote huku akiwashauri wenyeji kuepukana na utumizi wake na kuegemea biashara halali ya kusaka unga na kusaidia ujenzi wa taifa.