Aliyekuwa mwaniaji wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka huu Rueben Kigame ameitaka mahakama ya upeo inayohusika na kesi ya uchaguzi mkuu wa urais iweze kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi huo.
Akiongea na wanahabari mjini Eldoret,Kigame alisema hana imani na tume huru ya Uchaguzi na mipaka IEBC kwani anasema haikuandaa uchaguzi huru na wa haki hivyo haja ya uchaguzi huo wa urais kurudiwa kwa manufaa ya wakenya.
Wakati huo,aliwataka wakenya kukubali matokeo yatakayo tolewa na mahakama hiyo kesho na kuendelea kukumbatia mwito wa amani na kuishi kama watu wa jamii moja.