baraza la wazee:kaunti ni ya amani

Baraza la wazee katika kaunti ya Uasin Gishu wamedokeza kwamba kaunti ya hiyo ina amani ya kutosha kando na madai kwamba Kuna makaratasi za uchochezi ambazo zilisambazwa kaunti hiyo Jana.


Wakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza la wazee wa jamii ya Kaburwo John Yego na yule wa kisii David Nyambane walisema matamshi ya kuwepo Kwa makaratasi hayo ni kuwatia kiwewe wenyeji tu Kwa walichosema kaunti ina amani ya kutosha na hivyo wenyeji waweze kuendelea na shughuli zao bila ya kuhofu lolote.

Aidha,wazee hao wakizitaka idara husika za kiusalama kuchunguza madai hayo na kuwaadhibu washukiwa iwapo ni kisa cha uchochezi kwa mujibu wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *