Askofu wa Jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameiomba tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuhakikisha kwamba imeandaa uchaguzi wa huru na haki kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akiongea wakati wa hafla ya kusherehekea miaka 25 za padre Constantine Nyongesa Katika kanisa la Our Lady of Assumption Majengo Parish amesisitiza kuwa Imani ya wake ya wote imo mikononi mwa tume hiyo hivyo iwapo kuwatokea itilafu yoyote basi wakenya huenda wakakosa Imani na tume hiyo.
Askofu vilevile alisisitiza haja ya wakenya kuruhusiwa kuendeleza demokrasia Yao ya upigaji kura bila ya kuwekewa mashrati Kali na ngumu .
Aidha,askofu aliiomba idara ya usalama kutoa usalama kwa wakenya wote kwa usawa ndipo waweze waweze kushiriki vyema kwenye zoezi la uchaguzi huo.