Mwanamke mmoja ambaye ni mfanyikazi wa shirika la umoja wa kimataifa kuhusu chakula wfp(world food programme)mjini kakuma ameuawa kwa kuliwa na mamba katika ziwa turkana.
Mwanamke huyo alikuwa na wenzake wawili waliokuwa wakiogelea usiku mwendo wa saa tatu katika ziwa turkana kabla kukumbana na mauti.Inasemekana kwamba wenzake wawili waliponea kifo wakati mwezao alivutwa kighafla na mamba huyo ndiposa wakatoka ndani mwa ziwa turkana kwa haraka.
Wanawake hao walikuwa wanahudhuria kongamano la wiki moja katika hoteli moja kule turkana kabla ya mmoja wao kukumbana na mauti.Juhudi za uokozi zilitatizika jana usiku kwa sababu ya giza na mwili huo bado haujaweza kuonekana huku shughuli hizi zikirejelewa hivi leo.