SHA si ya mtu binafsi

Waziri wa afya Aden Duale ametoa onyo kali kwa wasimamizi wa hospitali nchini dhidi ya kushiriki utapeli wowote kwa kula njama ya kulaghai mamlaka ya jamii SHA kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Akizungumza akiwa ziara katika kaunti ya Uasin Gishu alisema kwamba hakuna pesa za ziada ambazo mkenya anapaswa kutozwa wakati wanatafuta huduma wakitumia SHA hivyo haja ya wao kuwa makini dhidi ya wakora hao.

Wakati huo,Duale alisema kwamba serikali imeweka mipango kambambe ya kupambana na maaumbikizi au hata kusambaa kwa ugonjwa wa Mpox ambapo Kaunti ya Uasin Gishu imeripoti kisa kimoja,akiwataka wakenya kuchukua tahadhari ili wasije wakaambukizwa au kusambaza ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *