Bishop Anyolo; Pendaneni ili muishi miaka mingi.

Wito umetolewa kwa wanandoa kuenzi familia walizojaliwa na mwenyezi mungu kwa kuwaelekeza vyema kiimani.

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Arnorld Subira Anyolo akihubiri katika parokia ya All Saints Riara wakati wa sherehe za Family Day,askofu Mkuu amewakumbusha wakristu kufahamu kwamba ndoa walizojaliwa ni kwa manufaa yao na pindi zinaposahaulika,kizazi cha kesho huenda kikakosa mwelekeo.

Wakati huo,askofu mkuu amewataka kina baba kuwatunza vyema kina mama waliopewa na mwenyezi mungu na wala sio kuwaweka kama watumwa akieleza kwamba,wao ndio wasaidizi kwao.

Amewataka kina mama nao kuwaheshimu wao zao na kuombea familia zao sizidi kusimama naye kristu.

Aidha,askofu Anyolo ametaka familia kumtegemeza mwenyezi mungu katika shughuli zao zote za familia ndipo familia hizo ziweze kusimama imara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *