Ukosefu wa maji Kapsowar

Wakazi wa Kapsowar eneo bunge la Marakwet magharibi kaunti ya Elgeyo Marakwet wameonyesha kughadhabishwa kwao hii leo kufuatia ukosefu wa maji.

Wakazi hao wanadai kuwa hilo limelemaza shughuli zao za kila siku huku wafanyikazi katika kichinjio wakilazimika kufunga chumba hicho.

Wakiongea baada ya kufika katika ofisi ya msimamizi wa wodi, wakazi hao wakiongozwa na Reuben Kibet wametaka serikali ya kaunti hiyo kuingilia kati suala hilo kwa dharura. Kwa upande wake msimamizi wa wodi hiyo James Komen amewahakikishia wakazi hawa kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa wamepata suluhu la kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *