Gavana wa migori okoth obado amejisalimisha asubuhi hii kwenye afisi za tume na maadili ya kupambana na ufisadi EACC.
Obado amejisalimisha katika afisi za eacc kisii kuhojiwa kuhusu madai ya kufujwa kwa zaidi ya shillingi million 73 pesa za umma.
Duru zinaarifu kwamba gavana Obado alifika katika afisi hizo akiwa pamoja na washukiwa wengine 9 wa kashfa ya ufisadi inayokumba serikali ya kaunti ya Migori
hivi sasa Obado na washukiwa wenzake wanahojiwa na makachero wa EACC wakitarajiwa kuwasilishwa mahakamani baadaye.
Mkurugenzi wa mashtaka Nordin Haji hiyo jana aliagiza akamatwe na kushtakiwa gavana Obado pamoja na watoto wake wanne na washukiwa wengine kuhusiana na kuporwa kwa mamillioni ya pesa kwenye serikali ya kaunti ya Migori ambayo Obado anaongoza.