KAKAMEGA – Wasichana wanufaika na msaada wa Sodo.

Zaidi ya wasichana hamsini kutoka kijiji cha Esiakula, eneo bunge la Matungu kaunti ya Kakamega, wamenufaika na msaada wa sodo miongoni mwa vifaa vingine kutoka kundi la vijana lilojiita; Kakamega Youth Leaders Stakeholders.

Kwa mujibu wa mratibu wa masuala ya vijana Halima Nyota, hatua hiyo ni katika juhudi za kuwasaidia wasichana wasioweza kupata sodo kwa urahisi kadhalika kuwaepushia mimba na ndoa za mapema.

Ameongeza kuwa wataendeleza mradi huo katika maeneo mengine ya kaunti ili kufikia walengwa.

Baadhi ya wasichana walionufaika na msaada huo wametoa wito kwa wenzao kujiepusha na mazingira yanayoweza kuchangia mimba za mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *