Askofu Tuka; Kanisa ni sehemu takatifu sio soko

Wanaisasa wameonywa dhidi ya kuandamana na wafuasi wao katika maeneo ya kuabudu nchini kama njia moja ya kukuza imani na kuzuia vurugu ambayo inashuhudiwa katika sehemu za kuabudu nchini.

Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka amesema kuwa kwa sasa taifa la kenya linahitaji amani akisikitikia visa vya makanisa kuvamiwa na wahuni ambao wanawawinda wanasiasa wanaohudhuria sehemu za kuabudu nchini, akiwakanya wanasiasa dhidi ya kuandamana na wahuni wanapoingia katika sehemu za kuabudu kama njia moja ya kuonyesha heshima kwa nyumba ya mwenyezi Mungu.

Ametoa wito kwa wanasiasa kadhalika kuchunga ndimi zao ili wasije wakatoa semi ambazo huemda zikachochea vurugu na uahasama miongoni mwa vikundi pinzani akitoa wito kwa wansiasa kunadi sera zao kwa amani pasi na vurugu.

Aslofu Oseso ametoa wito kwa vijana kadhalika kutokubali kutumiwa na wanasiasa wabinafsi kwa lengo la kuzua vurugu kwa kuwa vurugu hizo zinatishia mshikamano wa kitaifa n ahata kusambaratisha hali ya Uchumi nchini.

Amesema kuwa viongozi wanasthaili kuwa na hulka ya kusemezana na kusuluhisha miggoro kwa njia ya amani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *