MAENDELEO KWANZA

Rais William Ruto ametoa onyo kali kwa wakandarasi wanaochelewesha utekelezaji wa miradi muhimu ya serikali. 

Ruto alisema serikali imekusudia kutimiza ahadi zake kwa raia, akiongeza kuwa kuhujumu juhudi zao hakutavumiliwa.

Ruto aliyasema hayo leo Jumatano mjini Kisii ambako alikagua ujenzi wa Kituo cha Saratani cha Kisii.

Alielezea kutoridhishwa na hatua iliyopigwa katika utekelezaji wa mradi huo.

Rais Ruto alimwagiza mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kulingana na inavyotaka serikali la sivyo kandarasi hiyo ifutwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *