Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Lelei amewataka wazazi kuwa waangalifu na wanao wasije wakapotoka kimaadili .
Kulingana naye msimu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya huenda ikawanyima raha wazazi pindi wanao watakapojiingiza kwenye vikundi visivyostahili akidokeza kuwa,jukumu la mzazi sio kumpa mamlaka yote mwanawe ila kumwelekeza katika njia inayostahili.
Aliwataka wazazi hao kuchukua muda wao mwingi kuwapa sikio wanao ili iwapo wanapitia changamoto ya aina yoyote,waweze kuwapa mawaidha ya kutosha.
Askofu Lelei halikadhalika,amewataka watoto nao kuwa wenye heshima kwa wakubwa na wadogo ndipo shule zikifunguliwa warejelee masomo yao bila hitilafu yoyote.