Eldoret jiji la taka

Wakaazi jijini Eldoret wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Uasin gishu kuweka jaa la taka katika maeneo tofauti katika jiji, kama njia  moja ya  kuepukana na mrundiko wa taka kwenye maeneo yao ya kazi.

Wakiongea na wanahabari jijini humu wakaazi hao ambao  wengi wao ni  wafanyibiashara, wamesema kuwa taka imekuwa kero katika maeneo yao, na ni hatari kwa afya yao wakihoji kuwa hali hiyo imepelekea wengi kukosa wateja kutokana na hali duni.

Wakaazi hao kadhalika wametaka taa ziwekwe kwenye maeneo yao ya kibiashara kama njia moja ya kufanikisha biashara ya saa ishirini na halkadhalika kuwavutia wawekezaji wengi jijini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *