Sheikh Bini; siasa kando anguka nayo sasa

Viongozi wa kidini sasa wametoa wito kwa wanasiasa kuweka siasa kando na kufanya maslahi ya wananchi kipaumbele, kufuatia kukamilika kwa shughuli ya kuapishwa kwa Kithure Kindiki kama naibu rais.

Mwenyekiti ya baraza la dini ya kiislamu kaskazini mwa bonde la ufa Sheikh Abubakar Bini, amesema kuwa mchakato mzima wa kumbandua aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua ilipandisha joto la kisiasa nchini,  na kusababisha baadhi ya  huduma kwa wananchi kusitishwa.

Aidha viongozi hao wamemshauri naibu rais mpya Kithure Kindiki kudumisha uhusiano mwema na rais William Ruto, ili kuwatumikia wakenya jinsi inavyostahili, na kuwaleta wakenya pamoja kwa faida ya mshikamano wa kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *