Wakulima Wahimizwa kuweka mashamba tayari kwa upanzi

Huku msimu wa mvua ukikaribia, wakulima kutoka kaunti ya Elgeyo Marakwet wamehimizwa kutayarisha mashamba yao.

Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya hanga katika kaunti hiyo Simeon Cheptot ambaye amesema kuwa mvua kubwa utashuhudiwa kuanzia mwezi ijao na hadi mwezi wa sita.

Cheptot vile vile amewataka wakulima kuwasiliana na maafisa wa kilimo ili kuwashauri kuhusu mimea watakaopanda.Hata hivyo amewataka wakazi hawa kuhakikisha kuwa wametayarisha mitungi ya kuweka  maji ili kukabiliana na uhaba wa maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *