Padre mkuu wa jimbo katoliki la Eldoret William Kosgey amewataka wazazi kuwa karibu na wanao msimu huu wa sherehe za krismasi.
Akihubiri katika misa ya kufunga mwaka ya wafanyikazi wa jimbo la Eldoret,Kosgey alisema kuwa msimu huu una majaribu na changamoto si haba na hivyo wajukumike kikamilifu katika kuwapa wanao mwelekeo ulio bora katika jamii.
Kadhalika aliwahimiza kutafakari safari yao ya ukristo na kumtukuza mungu wanapojitayarisha kumkaribisha yesu maishani mwao pindi tu atakapozaliwa na pia kunyosha mkono wa msaada kwa wengine ili wapate Baraka na uzima wa milele.