BISHOP ANYOLO; TAFUTENI ROHO MTAKATIFU

Wakristu wametakiwa kuonyesha upendo kwa wenzao haswa msimu huu wa krismasi kwa kuwa upendo huo ndio dhihirisho ya ukristu.

Akihubiri katika kanisa la Consolata shrine jijini Nairobi kwenye misa ya kuadhimisha sakramenti ya kipaimara askofu mkuu amewataka waumini siku zote kujitayarisha kupokea roho mtakatifu ambayo humjaza mkristu na mapaji saba yakiwemo upendo.

Askofu mkuu kadhalika amesema kuwa roho mtakatifu humpa mkristu nguvu na ujasiri wa kukabiliana na changamoto ambazo kila kukicha binadamu hukumbana nazo, akitoa wito kwa kila mkristu siku zote kuishi maisha yanayomulikwa na roho mtakatifu.

Amewataka wakristu vilevile kujivunza kushukuru kwa vitu vidogo ambavyo Mungu amewajalia katika safari yote ya mwaka huu unaokaribia kuisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *