VIONGOZI WA DINI NCHINI WAMTAKA DPP KUSIMAMA KIDETE

Viongozi wa kidini nchini wametoa wito kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma Nooordin Hajji kusimama kidete katika vita dhidi ya usfisadi nchini .

Katika kikao na wanahabari viongozi hao walisema kuwa swala la ufisadi inarejesha nyuma juhudu za ukuaji wa uchumu wa nchi wakirejelea hatua ambapo mkurugenzi huyo alidai kuwa alitumiwa na serikali iliyopita kuwafungulia watu Fulani mashtaka ya kusingiziwa.

Wakati huo askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria aliwahimiza wakenya kupanda miti msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka ili kukabili mabadiliko ya tabianchi inayochangia ukame na njaa.

Muheria alisema kuwa chanzo kuu cha baa la njaa nchini imechangiwa kwa kiasi Fulani na ukataji ovyo wa miti jukumu ambalo ameutwika kwa wakenya wote kulinda mazingira kupitia zoezi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *