KOSGEY:tuko tayari kwa mazungumzo

Jamii Zinazoishi katika mpaka wa Bonde la Kerio wamesema wako tayari kukumbatia wazo la amani na kusitisha shughuli ya wizi wa mifugo.

Kwa mujibu wa afisa msimamizi wa haki na amani katika jimbo katoliki la Eldoret Samwel Kosgey ni Kwamba wakaazi waliandaa mkutano jana ,mkutano ambao alitaja kuwa nadhra sana kuandaliwa na ni wazi kwamba wenyeji hao wakao tayari kwa mazungumza za kupatikana kwa amani.

Kosgey vilevile akieleza kwamba wananchi hao waliwaomba wenzao kutoka maeneo hayo iwe ya Tiati na kaunti ya Baringo kwa Jumla,kaunti Pokot Magharibi,Elgeyo-Marakwet wakuwe tayari kuzuru eneo la kerio kwa anachosema wameleza wako tayari kuishi na wengine kwa amani.

afisa huyo alisema kwamba wenyeji hao wako tayari kufanya mazungumza hata serikali mpya kwa manufaa ya amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *