Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo aliwataka vijana kuimarisha imani yao kupitia kuiga mfano wa watangulizi wao wa kiimani.
Akiongea wakati wa hafla ya miaka 19 ya ukumbusho wa kadinali Maurice Michael Odunga aliwataka vijana hao kuiga mfano wake Odunga kwa alichowezesha taifa lake kristu kwa wanadamu na kuwawezesha wengine kupata mwongozo wake Yesu Kristu kwa matendo yake makuu wa kanisa.
Askofu huyo kadhalika aliwashauri wakristu kuwa mfano mwema kwa kizazi cha kesho ambao anasema wanahitaji mwelekeo mwema maishani mwao.
