Askofu wa kanisa la Jesus Love Ministries katika kaunti ya Uasin Gishu Wilson Kurui ameitaka serikali itakayochukua hatamu ya uongozi kuhangazia maswala ya maendeleo kwa wakenya wote bila ya ubaguzi wowote.
Akiongea mjini Eldoret,Askofu Kurui alieleza kuwa wakenya walishiriki uchaguzi kwa lengo la kuimarisha Ukuaji wa uchumi na iwapo azma hiyo haitatekelezwa basi watateseka sana na huenda wakakosa imani na uchaguzi nchini.
Wakati huo,Kurui aliwapongeza wakenya kwa kushiriki uchaguzi kwa njia amani akisema iliashiria wakenya kukua kuhusiana na uchaguzi na maamuzi yanayowaridhisha.