BISHOP KIMENGICH:Kubali matokeo

Viongozi wa kisiasa wametakiwa kukubali matokeo ya urais yatakapo tolewa na tume huru na uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Kwa mujibu wa askofu wa jimbo la Eldoret Dominic Kimengich, ni kuwa jukumu linalomilikiwa na IEBC ni la kipekee na sharti kila mkenya aiheshimu bila ya kuihitilafiana na shughuli zake.

Alisema wakenya wote walishiriki uchaguzi huo na uamuzi wa kingozi wanayemtaka na iwapo IEBC itamtangaza kiongozi ambaye wanasiasa hao hawakumuunga mkono haistahili wao kubabaika ila wakubali matokeo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *